Shule imeanza 01/01/1960 kama Bush School. Shule ilianza kutoa elimu ya dini ilijulikana kama Elimu ya Mungu na Wanadamu. Elimu hiyo ya dini ilitolewa na mwalimu Christian Namkoko Mnanjota mwenyeji wa Nanguruwe Newala.
Mwaka 1963 mwezi April shule ilisajiriwa kwa jina Rowa primary school chini ya uongozi wa Ndg Rifaustus Mng'oko kutoka chiwonga kama mwalimu mkuu. Mwaka 1964 alihamishiwa mwalimu Nambunga kama mwalimu mkuu msaidizi.
Majengo ya shule yalijengwa mwaka 1960 kama shule. Pia majengo hayo yalitumika kama Kanisa ambalo lilisimamiwa na Far.LAURENSI
Baadae shule iliendelea na kupata namba ya usajili MT/04/02/111 kama shule ya msingi Mcholi mwaka 1970.
Kumetokea mabadiliko mengi hapo awali. Miaka ya 1980s hadi 1990s shule ilikua katika kata ya Mkunya, baadae kata ya Mcholi.
Mwaka 1995 wilaya ya Newala iligawanywa na kupata wilaya ya Tandahimba hivyo shule ya msingi Mcholi ilikuwa katika halmashauri ya Tandahinba.
Baadae katika kufanya maboresho ya mipaka katika wilaya hizi mbili shule ikawa katika wilaya ya Newala.
Miaka ya 2000s kata ya Mcholi iligawanya na kupata kata ya Mcholi I na Mcholi II. Shule ya Msingi Mcholi II ilifuata jina la kata baada ya mabadiliko mengi yaliyofanyika miaka ya hapo katikati.
Mwaka 2015 halmashauri ya wilaya ya Newala iligawanywa na kupata halmashauri ya mji Newala na halmashauri ya wilaya ya Newala. Katika mgao huu shule ya msingi Mcholi II imepata namba ya usajili mpya ambayo MT/04/09/2290 kwa mabadiliko yalitokea mwaka 2017 sasa namba ya usajili inatambulika EM 2290.
MAHALI SHULE ILIPO.
Shule ya msingi Mcholi II ipo katika kijiji cha Msilili, Kata ya Mcholi II katika Halmashauri ya Mji Newala Mkoa wa Mtwara. Ni kama km 25 kutoka Newala.
WIMBO WA SHULE
Bonyeza hapa
WIMBO WA UZALENDO (TANZANIA)
Bonyeza hapa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni